Maandamano ya Amani Ubalozi wa Marekani

Taasisi ya Mtandao Rafiki kwa kushirikiana na CHAMATA pamoja na JUMIKITA tulifanya maandamano ya Amani kuelekea Ubalozi wa Marekani ili kushinikiza kampuni za Mitandao ya Kijamii zilizopo Nchini Marekani kuongeza umakini zaidi kwenye kufuatilia uhalifu wa kimtandao unaofanywa kupitia Mtandao wa Instagram, Facebook na X.

Uelewa mdogo wa lugha ya Kiswahili hususani kile kiswahili cha ndani na mtaani (slang) kunasababisha wahalifu wa kimtandao kufanikiwa kudanganya Akili Bandia na vitengo vinavyosimamia vigezo na masharti ya watumiaji wake.

Hatua hii ilifikiwa baada ya kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu wa kimtandao kutoka kwa mwanadada aishie Marekani aitwaye Mange Kimambi.