Kuhusu Mtandao Rafiki

Shirika lililojitolea kuboresha uelewa wa usalama wa mtandaoni na ulinzi kwa watumiaji wa mtandao na biashara ndogo na za kati (SMEs). Kupitia mipango na njia mbali mabli, tunajitahidi kuleta mabadiliko ya kudumu katika suala zima la ulinzi na usalama wa mtandaoni katika jamii yetu.

Tunatengeneza Mazingira Bora na Salama Mtandaoni kwa ajili ya wote.

Mtandao Rafiki imejizatiti kuboresha uelewa wa usalama wa mtandaoni na ulinzi kwa watumiaji wa mtandao na biashara ndogo na za kati (SMEs). Tunatoa elimu ya usalama wa mtandaoni kupitia warsha, kampeni za uhamasishaji na mwitikio wa matukio kwa SMEs. Shirika linapambana pia na utapeli wa mtandaoni kwa kuanzisha mifumo ya kuripoti na kutoa huduma za ushauri. Aidha, Mtandao Rafiki inafanya kazi ya kuzuia unyanyasaji wa watoto kupitia mipango ya elimu, ufuatiliaji na ripoti, na ushirikiano na mashule.

Misheni

Kuboresha uelewa wa ulinzi na usalama mtandaoni kwa watumiaji, kupitia elimu na utetezi, na kuunda mazingira salama mtandaoni kwa wote.

Maono

Kuwa katika mstari wa mbele katika kuelimisha jamii katika maswala yote ya ulinzi na usalama mtandaoni, ili kuhakikisha watu binafsi na biashara zinashamiri bila uoga wala wa vitisho au utapeli.

Maadili ya Msingi

Maadili yetu ya msingi yanaongoza dhamira yetu ya kuunda mazingira salama mtandaoni. Uadilifu, Uwezeshaji, Ubunifu, na Jamii vinaunda utamaduni na utendaji, kuhakikisha tunawalinda watumiaji binafsi na Biashara dhidi ya vitisho, huku tukikuza ulimwengu wa kidijitali wenye uaminifu na ushirikiano.

Uadilifu

Tunaendesha shughuli zote kwa njia inayodumisha sifa ya kuwa wakweli na waaminifu.

Kujenga Jamii

Kuunda jamii mtandaoni itakayo toa msaada na ushirikiano katita suala zima la usalama mtandaoni.

Ubunifu

Kuendelea kutafuta na kutekeleza mifumo mipya katika kupambana na changamoto za usalama wa mtandaoni.

Uwezeshaji

Kutoa ushauri, mbinu na maarifa ya kujilinda mtandaoni kwa watu binafsi na biashara.