Sheria Ya Ulinzi Wa Taarifa Binafsi 

Taarifa binafsi nyeti ni taarifa yoyote ambayo kwa mujibu wa Sheria za nchi inachukuliwa kama athari kubwa katika haki na maslahi ya mhusika wa taarifa. Taarifa hizi zinajumisha taarifa za vinasaba, taarifa za miamalaya kifedha, taarifa za kiafya. 

Taarifa Binafsi? 

Ni taarifa yoyote ambayo inaweza kutumika kumtambulisha mtu mahsusi kwa mfano jina kamili, anwani, tarehe ya kuzaliwa, namba ya hati ya kusafiriana namba ya leseni ya udereva. 

Taarifa binafsi nyeti ni taarifa yoyote ambayo kwa mujibu wa Sheria za nchi inachukuliwa kama athari kubwa katika haki na maslahi ya mhusika wa taarifa. Taarifa hizi zinajumisha taarifa za vinasaba, taarifa za miamalaya kifedha, taarifa za kiafya. 

Kwa mujibu wa Sheria taarifa binafsi hujuisha picha na video ya mtu fulani, mara kadhaa hapa Tanzania mahakama zimepokea kesi ya watu au taasisi kutumia picha ya mtu fulani kwenye tangazo bila ruhusa yake. Mfano mchezaji wa Simba John Bocco picha yake aliyopiga wakati wa mechi uwanja wa CCM kirumba-Mwanza ilitumika kwenye matangazo ya michezo ya kubahatisha bila ruhusa yake. 

TUJIULIZE MASWALI 

  • Ni lini taarifa zetu tulizotoa sehemu fulani mfano polisi, gesti na hotelini zinafutwa? 
  • Je, Zile jumbe fupi za makampuni ya kubet na michezo ya kubahatisha nani anawapa taarifa zetu mfano namba ya simu? 
  • Je, tunapo kwenda kwenye sherehe fulani mfano ndoa wale wapiga picha wanatuombaga ruhusa kabla ya kuanza kupiga picha? 
  • Je, taarifa tunazo toa wakati wa kusajiri kadi rasmi mfano kadi za benki, laini za simu na bima za afya zilikuwa na umuhimu na zinatumika Kwa kusudi husika? 
  • Kesho ukiamka asubuhi ukakuta picha yako imetumika kutangaza u bidhaa Fulani unajua unatakiwa kufanya Nini? 

Baada ya mabadiliko makubwa ya teknolojia imesababisha taarifa za watu kuwa ni Moja ya mtaji mkubwa kwa watu wengine na makampuni makubwa, hivyo Tanzania ikanona niwakati sahihi wa kutunga sheria rasmi ya kulinda haki kulindiwa taarifa binafsi. Lakini sio kulinda tu taarifa binafsi lakini pia kuhakikisha taarifa hizo zinamfaidisha Moja Kwa moja mlengwa wa taarifa endapo zinatakiwa kutumiwa Kwa matumizi fulani. 

Kabla ya sheria hii Tanzania ilikuwa ikitumia ibara ya 16 ya katiba na mikataba ya kimataifa Ili kulinda taarifa binafsi za watu lakini Sheria hizi zilikuwa na udhaifu mkubwa sana. Sheria imetungwa Kwa lengo kiwango Cha chini Cha matakwa ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi zinazo milikiwa na vyombo vya serikali na binafsi. 

UMUHIMU WA SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI 

  • Kudhibiti ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi 
  • Kuhakikisha ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi inafanyika Kwa kuzingatia misingi ya sheria 
  • Kulinda faragha za watu 

MISINGI YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI 

Sheria hii imeweka misingi rasmi ambayo mkusanyaji na mchakataji wa taarifa binafsi anatakiwa kuzingatia kwa umakini mkubwa Ambapo zimeongelewa kwenye kifungu Cha saba(7) Cha Sheria hii. 

  • Taarifa binafsi zinatakiwa kuchukuliwa kihalali, usawa na uwazi 
  • Zinakusanywa Kwa madhumuni mahususi 
  • Ni sahihi, zinaboreshwa, zinahakikiwa na kurekebishwa inapobidi 
  • Zinakusanywa na kuchakatwa Kwa kuzingatia haki ya muhusika 
  • Kuzingatia usalama wakati wote wa kuhifadhi 
  • Hazisafirishwi Kwa mtu au taasisi nyingine bila ruhusa ya muhusika 

CHOMBO CHA KULINDA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI 

Mnamo mwaka 2024 Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani aliteua na kuapisha wajumbe wa tume inayoitwa Tume ya Ulinzi wa taarifa binafsi ambayo Kwa mujibu wa Sheria kifungu Cha 10 imepewa majukumu yafuatayo 

  • Kufatilia utekelezaji wa Sheria twajwa 
  • Kusajiri wakusanyaji na wachakataki wa TAARIFA 
  • Ktupokea, Kuchunguza na Kushighulikia malalamiko kuhusu taarifa binafsi 
  • Kutoa adhabu kulingana na kosa 

MAKOSA NA ADHABU 

Sheria hii pia imeorodhesha makosa kadhaa na adhabu zake ikiwemo fani, vifungo vya jera na mara kadhaa vyote Kwa pamoja. 

SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO YA MWAKA 2015 

Ukuaji wa kasi wa teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Tanzania imepelekea mapinduzi makubwa sana kwenye sekta mbalimbali lakini kama ilivyo kwenye baadhi ya mambo Kila kitu kinakuja na changamoto basi Sheria hii imetungwa kuwa kizuizi Cha makosa yatokanayo na matumizi ya mtandao. 

Sheria hii inaweza kuwa na makosa kadhaa ambayo kwenye Sheria nyingine yapo tena yameelezewa vizuri kabisa mfano Sheria ya makosa ya jinai inayo makosa kadhaa kama wizi na ubaguzi lakini kilichofanya Sheria hii kutungwa ni kwasababu utendaji wa makosa kwenye mtandao ni tofauti na makosa yanayofanyika na kusimamiwa na Sheria nyingine. Makosa ya mtandao siyo lazima yafanyike ndani ya mipaka ya kijografia ya nchi husika na siyo lazima kitu lichoibiwa kihamishike. 

Sheria zilizokuwepo hapo mwanzo zilikuwa hazitambui makosa yanayofanyika kwenye mtandao hivyo kupelekea vyombo vya maamuzi kushindwa kutekelezwa wajibu wake, ni matakwa ya Sheria za nchi yetu Ili mtu adhibiwe ni lazima kosa lake lijulikane kisheria. 

AINA YA VITU/WATU WANAOWEZA KUPATA MADHARA KWA MAKOSA YA MTANDAO 

  • Mtu binafsi mfano kashfa na taarifa za uongo 
  • Taasisi mfano kuguashi kwaa kutumia komputa 
  • Mali mfano Matumizi ya Mali ya mtu pasipo na ruhusa 
  • Jamii mfano usambazaji wa ponografia na kamari za mtandaoni 

TUJIULIZE MASWALI 

  • Ni mara ngapi umekutana na taarifa za uongo za watu au taasisi maarufu? 
  • Ni mara ngapi umekuta na taarifa za kiongozi mkubwa kuwa anakopesha mikopo? 
  • Ni mara ngapi umesikia akaunti ya mitandao ya kijamii ya watu maarufu zimedukuliwa? 
  • Mara ngapi umesikia watu au taasisi wanatoa huduma ya kusoma jumbe za mpenzi wako? 
  • Mara ngapi umepata jumbe ya tuma kwenye namba hii au akaunti ya mtu maarufu ikitaka utumie fedha? 
  • Siku ukikuta mtu amesambaza video chafu mtandaoni unajua wapi kwenda kushitaki/kupeleka malalamiko? 

AINA YA MAKOSA YA MTANDAO 

Makosa ya mtandaoni yametengwa kwenye makundi manne(4) ambayo ni 

  1. Makosa dhidi ya kompyuta na mfumo wa kompyuta. 

Makosa haya mara kadhaa yamekuwa yakitajwa kwenye jamii zetu na Kwa lugha nyepesi tunasema udukuzi wa kompyuta ikiwa na maana ya kuingiria mfumo wa kawaida wa kompyuta bila ruhusa na kuwa na nia ovu. Udukuzi huu unaweza kufanywa kwa Nia ya kuiba taarifa, kuzuia taarifa na hata kuaribu kifaa.Mara nyingi makosa haya yanafanywa na watu wenyw uelewa mkubwa dhidi ya matumizi ya kompyuta Kwa sababu hutumia virusi fulani ilikukamilisha kosa. 

2. Makosa dhidi ya kutumia kompyuta 

Haya ni makosa ambayo mtu hutumia kifaa ambacho ni kompyuta Ili kitimiza lengo lake mfano wizi na utambulisho wa mtu binafsi, Kugushi nyaraka na udanganyifu. Mfano Mara kadhaa tumekutana na akaunti za mitandao ya kijamii za watu au viongozi wakubwa ikitoa taarifa za mikopo ambayo ukifatilia sio muhusika, Pia tumewahi kukutana na malalamiko ya watu kuibiwa nyimbo zao ambapo mtu mwingine amejimilikisha. 

3. Makosa dhidi ya maudhui 

Hapa ndipo watu wengi kama sio wote hutenda makosa haya labda Kwa kujua au kutokujua, mfano wa makosa hayo ni usambazaji wa ponografia, kashfa na taarifa za uongo na makosa uhaini, makosa ya unyanyasaji na ubaguzi Kwa kupitia mtandao. 

MAKOSA NA ADHABU ZAKE KISHERIA 

a)Kutoa taarifa za uongo faini ya sh. Millioni (5) au kifungo kisichopungua miaka (3) au vyote Kwa pamoja 

b)Kusambaza picha au video za ponografia faini isiyopungua millioni ishirini (20) au kifungu Cha miaka saba (7) au vyote Kwa pamoja 

c)Unyanyasaji kupitia mtandao faini isiyopungua millioni Tano (5) au jera miaka mitatu (3) 

CHOMBO KILICHOPEWA MAMLAKA YA MAKOSA YA MTANDAO 

Kama katiba ya Tanzania chini ya ibara ya 107(1)(2) na 30(3) mahakama imepewa nguvu ya kusikiliza na Kutoa maamuzi yote yanayohuru haki ya mtu au taasisi.